Posts

Showing posts from March, 2017

Walimu, Ninyi ndio Mnaojifunza, Wanafunzi wenu ni Wapokea Taarifa tu

Image
                                            Picha kwa hisani ya www.jiandae.wordpress.com                                                                               Kuna msemo usemao, kati ya anayefundisha na anayefundishwa, anayejifunza zaidi ni yule anayefundisha/ elekeza. Msemo huu una ukweli kwa kuwa, anayefundisha hujiandaa kwa kila hali na pia kupata fursa ya kutumia kile alichojifunza kwa kuelekeza wenzake. Msemo huu bila shaka, chanzo chake ni aina ya ufundishaji wa muda mrefu uliozoeleka mashuleni. Kwamba, mwalimu ndiye anayepaswa kusoma kwa kina na kisha kuwaeleza wanafunzi dhana ya yale aliyoyasoma. Kimsingi, mwalimu anatoa taarifa ya alichojifunza kile wanafunzi wanachopaswa kukijifunza.   Bila shaka unaweza ukashangazwa au kupata mshtuko, lakini hali halisi ndio hii. Kabla ya kufundisha, mwalimu anapaswa kujiandaa na somo. Kwa mtazamo wa ufundishaji wa walimu wengi, jukumu lao kubwa ni kujisomea ili wapate uelewa wa kutosha kuhusu kile wanachopaswa kuk

Mbinu za Kusaidia Kujenga Utamaduni wa Ufundishaji wa Kiudadisi Mashuleni

Image
                   Picha kutoka tovuti ya Linkedin Moja ya changamoto zinazokwamisha matumizi ya ufundishaji wa kiudadisi mashuleni ni hali ya utayari wa walimu, wakuu wa shule, viongozi wa kisiasa na wadau wengine wa elimu.  Changamoto kadhaa zinatajwa kukwamisha utekelezaji wa ufundishaji na ujifunzaji huu. Baadhi zikiwemo uhaba wa nyenzo za kujifunzia na walimu kukosa maarifa ya namna ya kutumia njia za ufundishaji zainazoendana na matakwa ya mfumo huu.  Hata hivyo, katikaki ya changamoto hizi, bado utekelezaji wa ufundishaji na ujifunzaji huu unawezekana. Utayari wa wadau wa elimu ndio chachu pekee ya kufanikisha hili. Palipo na utayari, changamoto kama hizi huweza kuonwa kama fursa na kuzifanyia kazi na hatimaye kufanikisha utekelezaji wa ufundishaji unaowazingatia wanafunzi. Ni heri mwalimu wa darasa la wanafunzi 50 aliye na kitabu kimoja na nia thabiti ya kutafuta namna ya kuwapa wanafunzi kitabu hicho wajifunzie, kuliko mwalimu wa darasa kama hilo aliye n

Ufundishaji wa Kiudadisi: Maana, Faida na Namna Unavyoweza Kutumiwa

Image
                                           Picha kwa hisani ya UNESCO learning Portal Matumizi ya njia ya ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi umeenea maeneo mbalimbali duniani na hususani katika nchi za Ulaya. Ufundishaji Unaomzingatia Mwanafunzi ni mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji unaompa mwanafunzi fursa ya kujibidisha ili kujipatia maarifa na kutumia maarifa yake ya awali katika kujenga maarifa mapya badala ya kuwa mpokeaji wa maarifa na kisha kuyatumia kwa namna ya kuyakariri.     Katika machapisho mbalimbali, Ufundishaji Unaomzingatia Mwanafunzi umekuwa ukipewa majina anuai kama vile ufundishaji shirikishi, ufundishaji unaomzingatia mtoto, ufundishaji wa Kiudadisi na majina mengine. Hata hivyo, watumiaji wengi wa mfumo huu wa kufundishia na kujifunzia wanatumia zaidi istilahi ya Ufundishaji wa Kiudadisi. Ufundishaji wa Kiudadisi bila shaka ni istilahi pendwa kwa kuwa inasadifu moja ya tabia muhimu ya udadisi anayopaswa kuwa nayo mwanafunzi wakati wa ujifunza

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"