TUZO ZA WALIMU BORA TANZANIA 2012-2013


Naam, ni habari njema kwa walimu wa Tanzania. Tulizoea kuziona tuzo nyingine mbalimbali kama zile za waandishi wa habari na zile za wanamuziki (Kilimanjaro Music Awards), sasa umefika wakati wa kushuhudia tuzo za Waalimu bora Tanzania. Ni tukio la kipekee na la kihistoria hapa Tanzania.

Kwa mujibu wa kamati ya uratibu wa tuzo hizi inayoongozwa na ndugu Clemence A. Kambengwa, tuzo hizi zinaandaliwa na asasi iitwayo  EDUCATION AND EXPEDITION AGENCY ASSOCIATION.

Taarifa ya Kamati ya Uratibu ya tuzo hizi inaendelea kueleza kuwa, tuzo hizi za kihistoria hapa nchini zitashirikisha walimu wa shule za msingi na shule za Sekondari kutoka nchi nzima. Mchakato unaendelea, ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa taratibu zote za maadalizi. Taarifa rasmi kuhusu zawadi zitatolewa wakati wa uzinduzi ila matarajio ya zawadi kwa washindi zitakuwa ni zawadi za aina yake ambazo hazijawahi kutolewa hapa nchini.

Uzinduzi rasmi wa Tuzo hizi unatarajiwa kufanyika Nov 20/2012 na kilele chake itakuwa ni Tarehe 25/NOV 2013.

Taarifa zaidi zitazidi kutolewa kuhusiana na tuzo hizi.

Taarifa hii (kama nilivyotangulia kutaja) ni kwa mujibu wa Kamati ya Uratibu ya tuzo hizi za kihistoria za Walimu inayoongozwa na ndugu Clemence A. Kambengwa (Event Director, info@eeaa.or.tz/0762000505)


 


 


Comments

Amos Msengi said…
Ha ha ha ha haaaaa............ hizo tuzo ni kiini macho wajanja wachache wale donge zito kisha watumishi waukweli wataishia kusikia tu. Sijasikia ushirikishwaji wa huo mchakato kaka.
WEB CREWS INC said…
Fuatilia sasa kama bado hujapata habari za shirikishwaji inabidi uwe mtu wa mtandao na kusikiliza vipindi redio TV

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"