Posts

Showing posts from June, 2012

TUZO ZA WALIMU BORA TANZANIA 2012-2013

Image
Naam, ni habari njema kwa walimu wa Tanzania. Tulizoea kuziona tuzo nyingine mbalimbali kama zile za waandishi wa habari na zile za wanamuziki (Kilimanjaro Music Awards), sasa umefika wakati wa kushuhudia tuzo za Waalimu bora Tanzania. Ni tukio la kipekee na la kihistoria hapa Tanzania. Kwa mujibu wa kamati ya uratibu wa tuzo hizi inayoongozwa na ndugu Clemence A. Kambengwa, tuzo hizi zinaandaliwa na asasi iitwayo  EDUCATION AND EXPEDITION AGENCY ASSOCIATION. Taarifa ya Kamati ya Uratibu ya tuzo hizi inaendelea kueleza kuwa, tuzo hizi za kihistoria hapa nchini zitashirikisha walimu wa shule za msingi na shule za Sekondari kutoka nchi nzima. Mchakato unaendelea, ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa taratibu zote za maadalizi. Taarifa rasmi kuhusu zawadi zitatolewa wakati wa uzinduzi ila matarajio ya zawadi kwa washindi zitakuwa ni zawadi za aina yake ambazo hazijawahi kutolewa hapa nchini. Uzinduzi rasmi wa Tuzo hizi unatarajiwa kufanyika Nov 20/2012 na kilele chake itaku

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"