Mwonekano wa kilele cha mlima Kilimanjaro kulingana na mahali mtu alipo mkoani Kilimanjaro.
Muonekano wa kilele cha mlima Kilimanjaro kwa hapa mkoani Kilimanjaro hutegemea na mahali unapouangalia mlima huu. Wilaya ya Moshi(mjini na vijijini), Rombo, na baadhi ya maeneo wilayani Hai, (Siha, Mwanga na Same sijawahi ku-view mlima Kilimanjaro hivyo sitaweza kuzungumzia mwonekano wa kilele cha Mlima kwa sasa. Pengine mwonekano hautatofautiana na wa Rombo au Moshi) kilele cha mlima huonekana kama jinsi picha inavyoonyesha hapo juu.

Kwa baadhi ya maeneo kama Masama wilayani Hai na baadhi ya maeneo mkoani Arusha yanayopakana na mkoa wa Kilimanjaro. mwonekano wa kilele cha mlima ni tofauti kwani pale juu kabisa kunaonekana kuna bonde, kiasi kwamba mtu aliyeko Masama N'guni mathalani, akiambiwa achore kilele cha mlima kwa kadiri ya namna akionavyo kilele, atachora kama kinavyoonekana kwenye picha hapa chini.Nashindwa kuelewa ni kwa nini kilele ambacho ni "Iconic" ndicho ambacho huonyeshwa na hutumika zaidi kwenye picha na maonyesho mengi yahusuyo mlima huu. Kama sikupata fursa ya kufika Masama wilayani Hai kijijini Ng'uni, nisingekaa kujua kuwa mwonekano wa kilele cha mlima unatofautiana kutegemea na mahali mtu alipo ktk mkoa wa Kilimanjaro kwani nilizoea kuona kilele cha mlima ambacho ndicho hicho hicho nilichozoea kukiona hata kwenye picha.

(samahanini picha hazijakuwa na mwonekano mzuri sana)

Comments

Bila samahani kaka ni picha nzuri kwa kweli tuna haki ya kujivunia mlima wetu. Ahsante kwa kutuonyesha mwonekano tofauti!!
Albert Kissima said…
Hakika dada Yasinta, hatuna budi kujivunia kivutio hiki chenye ushawishi mkubwa kote duniani. Tujivunie kwa kuupanda mlima huu na pia mapatato ya mlima huu yatumike vizuri kwa manufaa ya taifa na wananchi, na hapa ndipo pia tutajivunia zaidi na zaidi.
Bennet said…
mlima wetu jamani unaowafaidisha wenzetu, na hii jumuiya mpya mbona tutalala njaa
Albert Kissima said…
Da! Ni kweli kaka Bennet, si kufaidi kwenye vivutio tu, bali hata sehemu nyingine nyingi kama za kielimu n.k, tusipokuwa imara watatupiga mieleka isiyohesabika.
José Ramón said…
Halaaaaa Interesting! Post. HONGERA! ...

Salamu kutoka kwa ubunifu na photos mawazo ya José Ramón
Albert Kissima said…
Nashukuru sana José, salamu zimefika na karibu tena na tena hapa "Mwangaza"

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija-Sehemu ya Pili