Lijue na hili
Wakati mwingine wanyama(wafugwao majumbani na hata wale wa kwenye hifadhi) wanapopatwa na matatizo(mfano ugonjwa), inakuwa vigumu kutambua. Kwa kiasi kikubwa unahitajika utaalamu na uzoefu ili kuweza kugundua mapema kabla hali haijakuwa mbaya na hata kupelekea kumpoteza mnyama.


Je, wafahamu dalili ya awali kabisa pale ng'ombe anapokuwa amepatwa na ugonjwa fulani?


Kama unajua,ni vema,utanisadia kuboresha,na kama ulikuwa hujui,basi, ni wakati wako mzuri wa kujifunza.


Kwa kawaida ng'ombe mwenye afya njema pua yake huwa na unyevunyevu wakati wote. Kwa ng'ombe ambaye ameanza au anayeshambuliwa na ugonjwa, pua yake huwa kavu kabisa. Kwa hiyo pindi uonapo pua ya ng'ombe imekuwa kavu, chukua hatua za haraka za kumuita mtaalamu kwa uchunguzi zaidi na matibabu.

Comments

Fadhy Mtanga said…
Ahsante sana kaka kwa darasa hili. Mimi siku zote nilidhani pua ya ng'ombe ikiwa na unyevu basi ngombe iyo iko gonjwa. Kumbe sivyo.
Albert Kissima said…
Ndio hivyo kaka, ng'ombe akiwa na unyevu kwenye pua ni dalili nzuri sana ya kuwa hana tatizo, hususani ugonjwa.
Hata mie nilidhani kama mtani Fadhy Ahsante sana kwa darasa zuri
Wasilojua baadhi ya watu ni kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo kuonekana vibaya ndio uzuri wake.
Mtoto akizaliwa na asipolia basi watu watakuwa na mashaka na watajitahidi kumfanya alie.
Milango ikibamizwa siku za mwanzo za maisha ya mtoto na asishutuke basi kuna wasiwasi na uwezo wake kusikia.
Sasa umenipa hii ya "constant flu" ya ng'ombe kuwa ni kitu chema.
Great darsa.
Blessings
Albert Kissima said…
Dada Yasinta nami nashukuru,

Kaka Mubelwa, usemacho ni kweli. Hata ng'ombe azaapo,nimeshuhudia vyuma vyenye sauti kali vikipigwa, na lengo hasa ni kumfanya ndama alie.
Bennet said…
Wakati jua la asubuhi linapotoka angalia ngozi za ng'ombe wako kama zinakuwa na rangi ya kahawia na zinang'aa au kumeta meta basi ujue washaambukizwa ndorobo na mbung'o wanahitaji dawa zizi zima hata kama si wote wanaumwa
Albert Kissima said…
Shukrani tena na tena kaka Bennet, ni darasa zuri kwa hakika. Wanablog na jamii kwa ujumla tunafurahia uwepo wako.
Albert Kissima said…
Shukrani tena na tena kaka Bennet, ni darasa zuri kwa hakika. Wanablog na jamii kwa ujumla tunafurahia uwepo wako.

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija-Sehemu ya Pili