Posts

Namna ya Ujifunzaji ni Moja ya Changamoto kuu ya Elimu Yetu.

Image
Mwalimu Hottish wa Shule moja huko Ghana Akichora Kitumizi cha Microsoft Word kama namna ya kuwasaidia wanafunzi wake kujifunza. Picha kwa hisani ya www.MillardAyo.com Mjadala wa kujadili mustakabali wa Elimu yetu umeitishwa. Bila shaka ni kutokana na mwenendo usioridhisha wa elimu yetu.  Elimu yetu inaonekana kutokukidhi mahitaji ya watanzania na Taifa kwa ujumla. Hata hivyo, kabla ya kufika mbali, wadau wa elimu-walimu, wanafunzi, wazazi, raia, viongozi, n.k wanafahamu bayana kuhusu matarajio ya elimu inayotolewa? Kwa mini tunasema   elimu yetu imezorota? Wanafunzi kufeli sana? Mazingira ya kufundishia na kujifunzia kuwa magumu (sana)? Tunahitaji elimu itusaidie kufika wapi kama watanzania na kama Taifa?Pengine maswali haya yabaki kama sehemu ya kuchochea mjadala wa wa kitaifa kuhusu elimu nchini kwetu.  Makala haya yanalenga kushirikisha uzoefu wangu wa darasani na kuonesha angalao moja ya maeneo ambayo, yakifanyiwa kazi vizuri, yanaweza kuifanya elimu yetu ikapigiw

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani? Sehemu ya Pili.

Image
Picha kutoka Mtandaoni na kuboreshwa na mwandishi wa Makala haya. Katika makala iliyotangulia, nilijadili mambo makuu mawili ambayo walimu na wanafunzi wanapaswa kuyafanya ili kuendana na mfumo wa ufundishaji unaomzingatia mwanafunzi. Mamo haya mawili ni wajibu wa mwalimu na mwanafunzi na malengo ya maudhui yanayofundishwa. Makala haya yanalenga kuendelea kujadili namna nyingine tatu zinazoweza kuzingatiwa na walimu na wanafunzi ili kufanikisha utekelezaji wa mitaala inayomzingatia mwanafunzi. Kwenye makala haya, tutaaangalia wajibu wa kujifunza, nafasi ya mwalimu na mwanafunzi kuhusu masuala ya ujifunzaji na malengo ya upimaji wa mwanafunzi. Wajibu wa Kujifunza.  Wajibu wa kujifunza ni hali ya utayari wa mwanafunzi kushiriki kwenye mchakato wa ujifunzaji bila kulazimishwa ama kushurutishwa. Hali ilivyo sasa, wanafunzi wanafahamu wajibu wa mwalimu ni kuleta maarifa darasani na wajibu wa wanafunzi ni kumsikiliza mwalimu na kuandika nukuu.  Katika mfumo huu, mwalimu ndiy

Kubadilika kwa Mitaala: Walimu na Wanafunzi Wabadilike kwa Namna Gani?

Image
Kila mwanafunzi anajituma wakati wa kujifunza katika harakati za kufikia malengo yao ya ujifunzaji. Picha: Mwandishi wa makala Kama mnakumbuka, kati ya mwaka 2005 na  2007 yalitokea mabadiliko ya mitaala, hususani kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya Ualimu. Kulikuwa na msemo uliovuma sana wa "muhamo wa ruwaza" au "paradigm shift" kwa kiingereza. Ruwaza ni mfumo au imani inayomuwezesha mtu kutekeleza jambo fulani kulingana na matakwa na taratibu fulani zinazofahamika. Kwenye ufundishaji, iliaminika kuwa mitaala yetu ilikuwa ya mfumo unaomuona mwalimu kama chanzo cha maarifa na mwanafunzi kama pipa linalosubiri kujazwa tu maarifa. Mitaala mipya inaaminika kuwa ya ruwaza tofauti, ndio maana mabadiliko haya yakaitwa ya kuhama kwa ruwaza. Namna mitaala ilivyoandikwa na namna ya kuitekeleza ni miongoni mwa mabadiliko haya. Kwa mfano, mabadiliko haya yalipelekea maandalio ya masomo yawe na kipengele cha upimaji kwa kila hatua ya somo. Pia, zimependekezw

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija-Sehemu ya Pili

Image
Mambo makuu ya kuzingatia ili kufanikisha upimaji endelevu wenye tija. Picha: Mwandishi wa Makala. Hakuna mjadala kuwa upimaji endelevu ni sehemu muhimu sana wakati wa mchakato wa kufundisha na kujifunza. Taarifa za namna ufundishaji na ujifunzaji unavyokwenda zinategemewa kupatikana kupitia upimaji endelevu bora. Makala haya yanalenga kuendelea kujadili mambo makuu manne kama tulivyoyaona katika makala iliyotangulia. Mambo hayo ni ufafanuzi wa kina wa mambo makuu yanayopaswa kujifunzwa na wanafunzi (clarifying learning), kuwajengea wanafunzi ari ya kujifunza (activating learners), kutoa mrejesho wa maendeleo yao (providing feedback) na kutafuta ushahidi wa ujifunzaji (eliciting evidence of learning). Katika makala haya nitajadili utoaji wa mrejesho wa Shughuli za Ujifunzaji (providing feedback) na utafutaji wa ushahidi wa ujifunzaji (Eliciting evidence of learning). Kutoa Mrejesho wa Shughuli za Wanafunzi (Providing Feedback) Kila anachokifanya mwanafunzi, anatamani sana

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Image
Picha: Blogger. Upimaji endelevu wa mwanafunzi ndio namna pekee ya kutoa taarifa za maendeleo ya ujifunzaji wa mwanafunzi katika kufikia malengo ya ujifunzaji yaliyokusudiwa kwake. Kwa hiyo, upimaji endelevu ni shuhguli ya msingi mno ya kuzingatiwa na mwalimu na wanafunzi.  Upimaji endelevu siyo shughuli ya mwalimu peke yake. Ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na manafunzi. Hii ni kusema kuwa, upimaji endelevu ni sehemu ya ujifunzaji wa mwanafunzi na ufundishaji wa mwalimu. Ikiwa tunahitaji kuona upimaji wenye tija, basi kila mmoja ni lazima atimize wajibu wake kwa kushirikiana. NWEA katika chapisho lao la mwaka 2016 linaloelezea mambo makuu manne ya kuzingatia ili kuleta ufanisi kwenye upimaji endelevu, wanaeleza kuwa upimaji endelevu   ni mchakato wa pamoja kati ya mwalimu na wanafunzi wa kukusanya ushahidi wa ujifunzaji wa wanafunzi kwa lengo la kuboresha kile kinachoendelea darasani, kwa maana ya mchakato wa ujifunzaji wa wanafunzi.   Ili kufanya mchak

Popular posts from this blog

Mambo Makuu Manne ya Kuzingatia ili Kufanya Upimaji Endelevu Wenye Tija

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuboresha na Kuongeza Ufanisi wa Shule.

Mmea wa Mlonge- "Moringa Oleivera"